____________________ Kampuni ilifungua kazi mwaka 2021 ikiwa na wafanyakazi 17 wakujitolea, idadi iliongezeka kulingana na mahitaji ya kazi, mpaka kufikia mwaka hui 2024 jumla ya wafanyakazi 350 wameshapitia kufanya kazi kwenye kampuni. Idara inayoongoza ni ya kilimo 75%, umeme 12%, uzalishaji samaki 10%, kusaga na kukoboa 8% na ofisini 5%.
Idadi iliyopo kazini msimu wa leo Agosti-Septemba 2024 ni 188.
____________________
____________________ SOFIJEP SARL KAMPUNI RAFIKI WA ULINZI WA MAZINGIRA
Kwa jumla kampuni inatoa nafasi ya heka 600 kupanda miti 220,000. Hii ni miti ya kawaida 100,000 aina ya mikaratusi na aina nyingine na ile ya matunda ni 120,000 miparachichi, machungwa, maembe na machenza. Idadi hii itaifanya kampuni kushikilia nafasi ya kwanza katika hali ya kuifadhi mazingira kwa njia ya upandaji miti tarafani na mkoani. Ni mategemeo yetu kuwa fursa hii itatoa nafasi ya kampuni kuwa mdahu mshiriki wa kongamano, ruzuru na mikutano inayohusu mazingira tarafani, mkoani hata ndani ya nchi. ____________________
Soma zaidi kuhusu shughulizilizopo na na miradi iliyoendelea