SOFIJEP SARL ni kampuni ya kibiashara ya kuzalisha bidhaa za kilimo na ufugaji ambayo iko na makao yake makuu tarafani fizi ndani ya mkoa wa sud-kivu katika nchi ya Kongo-Kinshasa.
kampuni hii imeanzishwa mnamo mwaka 2021 na kijana mzalendo na mzawa wa tarafa hili la Fizi ndugu Ekyoci Pendelelo Kicho kwa malengo makuu ya kuleta maendeleo tarafani, kutengeneza nafasi za ajira kupitia shughuli, mchanganyiko kwa kuanza na kilimo, ufugaji wa samaki, nyuki na kuku, huduma mbalimbali za umeme na uchapishaji na kutengeneza juice, kusindika vyakula na bidhaa tunavyozalisha kwa mfumo wa biashara.
Pamoja na kuwa na program nyingi za kilimo cha mda mrefu kama machungwa, chenza na embe lakini kampuni imeifanya parachichi (Avocat) kuwa kilimo chake cha kipau mbele kwa sababu zaidi za kibiashara, ki afya, kimazingira kwa kutengezea juisi na faida zingine ambazo zinaletwa na mmea huu.
Mnamo mwaka 2023 katika hali ya kusaidia serikali na mashirka kupunguza njaa nchini kampuni ilianzisha program ya kuongeza chakula kwa ulimaji wa mahindi, maharage na kalanga kama njia ya kupunguza njaa kwa kusimika kiwanda cha kisasa cha kukoboa na kusaga unga wa dona na sembe kwa viwango vinavyohitajika.
Bila shaka hamasa inatiya moyo na kuleta hamu na nia ya kuendelea licha ya kuwepo na changamoto nyingi za ki miundombinu na ki uchumi pamoja na mazingira magumu ya uwekezaji katika nchi yetu ambamo sekta isiyo rasmi haikubaliki na upatikanaji mitaji umeverugwa: Fikiria kwa mfano mahitaji ya umeme katika kuendesha mitambo na mashine mbalimbali za kampuni yametufanya kuanza huduma za kufua umeme kwa matumizi ya kampuni pamoja na kuhudumia jamii ya Fizi na viunga vyake.
Katika hali ya kuthaminisha sekta isiyo rasmi, kupata mtazamo mpya, ki-kazi na ki-ajira kwa lengo la kuinua uchumi wa inchi na wakaaji
SOFIJEP SARL iliamua kufuata taratibu na njia za utendaji zilizopendekezwa na OHADA kama ilivyoidhinishwa ndani ya sharia inayoongoza makampuni nchini Kongo na Afrika ili kufikia malengo ya uendeshaji kampuni kwa:-
MOTISHA NA MSUKUMO (MOTIVATIONS)
Pamoja na nia yakuleta maendeleo nyumbani, pamoja na mapungufu na changamoto za kiuchumi na ki miundombinu kuanzisha na kusimamisha kampuni katika mazngira magumu yakuwekeza nchini na tarafani kwetu, msukukumo wa kuanzisha kampuni ya kibiashara na uzalishaji ulitokana na roho ya uzalendo baada ya kuhamasika na fursa zilizopo ndani ya tarafa yetu ya Fizi :
SOFIJEP SARL KAMPUNI RAFIKI WA ULINZI WA MAZINGIRA
Kwa jumla kampuni inatoa nafasi ya heka 600 kupanda miti 220,000. Hii ni miti ya kawaida 100,000 aina ya mikaratusi na aina nyingine na ile ya matunda ni 120,000 miparachichi, machungwa, maembe na machenza. Idadi hii itaifanya kampuni kushikilia nafasi ya kwanza katika hali ya kuifadhi mazingira kwa njia ya upandaji miti tarafani na mkoani. Ni mategemeo yetu kuwa fursa hii itatoa nafasi ya kampuni kuwa mdahu mshiriki wa kongamano ruzuru na mikutano inayohusu mazingira tarafani, mkoani hata ndani ya nchi.
CHANGAMOTO ZA KUSHUGULIKIA (Chalenges) :-
Kuboresha bidhaa, kuongeza mtaji ili kukidhi mahitaji ya soko.
Kushawishi makampuni makubwa kuunua bidhaa za kampuni.
Kuhimiza mashirika ya serikali kutoa kipaumbele kwa makampuni ya ndani
.
Serikali kuboresha siasa ya mazingira ya uwekezaji nchini pamoja na kuboresha miundubino barabara, umeme na maji.
KUANZISHA NA ANWANI YA MAKAO MAKUU
Kampun ilianzishwa mnamo mwaka Juni 2021, apa Fizi.
Tunapatikana Fizi Centre, Cite Belge, Quartier Abunda, Groupement Babungwe Sud, Secteur Ngandja, Territoire de Fizi, Province du Sud-Kivu en Républiques Démocratique du Congo
Ukihitaji mengi download : Fiche d’information ya kampuni (PDF doc 1)
PROFILE GENERALE DE LA SOFIJEP