MENGINEYO

UTAFITI WA MAZINGIRA NA FURSA ZA UENDESHAJI SHUGHULI ZA KAMPUNI

Etude Du Milieu Et Faisabilité des Actions de da Société

Baada yakujifunza mazingira ya kuanzisha kampuni na miradi ya uzalishaji na biashara ndani ya na nje ya tarafa ya Fizi, tumejifunza kuwa :


Wateja, Bidhaa Na Beyi, Upinzani Wa Soko (Concurrence Du Marche) :


Kwa hatua hii hakuna upinzani wowote katika eneo la utendaji wa kazi zote na shughuli za kampuni ambazo zinaweza kuletea kampuni changamoto hali hii isichukuliwe kama chanzo cha uzembe ili kubweteka kufikia malengo ya mafanikio yanayohitajika lakini kama fursa ya kujenga jina kuwa kubwa kwa kuteka soko la ndani hata nje ya nchi.


Walengwa (Cible):

Wateja walengwa wa biashara zetu ni wananchi, wafanyabiashara, ma hoteli, bar, migahawa, wasafiri, na makampuni ya ndani na nje ya nchi pamoja na mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi, ya kitaifa na kimataifa.


Miradi (Nature des projets):

Miradi yote ni ya kibiashara na ya kudumu, itaanza kwa kiasi kidogo na baadaye na itasambaa na kukuwa taratibu maeneo mengine.


Kuchagua miradi iwe aina ya kudumu na ihusike na mahitaji ya matumizi ya kila siku (Parachichi, Machungwa, Maembe, Machenza, unga wa mahindi, Maharagi, Kalanga, Samaki, Kuku, mayayi, Umeme) n.K


Ili kuingeza uzalishaji pia kampuni itatengeneza program maalum ili kununua mazao ya wakulima wengine.

ADDRESS

Drc Congo, Kinshasa

Sud-kivu, Fizi.

Phone: + (243) 912 911 445

Phone: + (243) 994 878 164

Email: info@sofijep.com

Copyright © 2024 Sofijep SARL All right Reserved